top of page

Kazi imeanza msimbazi, Hassan Dalali ashiriki kikao maalumu cha kuiua Yanga

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 21, 2015
  • 1 min read

Kazi imeanza. Hatimaye, Simba imepata ‘sumu’ hatari ya kuiteketeza Yanga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa wikiendi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Simba imeipata sumu hiyo baada ya juzi Jumamosi kukaa kikao kizito kwa saa nne kilichoitishwa na wakuu wa matawi yote ya timu hiyo kujadili na kutafakari jinsi ya kumfunga mpinzani wao huyo, huku mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Hassan Dalali naye akishiriki kikao hicho.

Msimu uliopita katika michezo yote miwili ya ligi, Simba ilifanikiwa kuvuna pointi nne baada ya kutoka suluhu mchezo wa kwanza, kisha kuifunga bao 1-0 katika mchezo wa pili.

Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa ambao ndiyo walikuwa waandaaji wa mkutano huo, Ostadh Masoud, alisema kuwa walilazimika kuitisha kikao hicho cha dharura haraka ili kujadili mapema jinsi ya kuifunga Yanga.

Alisema kuwa katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Annex Lango la Jiji na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Simba akiwemo mwenyekiti wa zamani Dalili, walikubaliana kuwa kwa sasa kila mwanachama aifikiria kwa makini mechi hiyo pamoja.

Aliongeza kuwa mara baada ya kikao kumalizika, kila mmoja aliondoka na jambo moja tu la mshikamano, nguvu, umoja na kuahidi kuwa watapambana kadiri wawezavyo ili kuifanikisha timu yao ipate ushindi.

“Tulichokijadili ni jinsi gani tutaweza kumpiga Yanga kama ilivyokuwa msimu uliopita na tukakubaliana kuwa katika kipindi hiki tuwe na mshikamano, umoja, tujenge nguvu moja kwa kushirikiana kuiangamiza Yanga.

“Rais Aveva (Evans) tulimuita kwenye kikao hicho, alikuja ila kutokana na majukumu mengine hakukaa hadi mwisho, lakini tulikuwa na viongozi nguli kama mzee Dalali na Bi Hindu ambao hao ni wazoefu na mechi za Yanga, tumekubaliana vizuri na yote tuliyokubaliana tumeyapeleka kwenye uongozi wa juu,” alisema Masoud.


 
 
 

Comentários


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page