top of page

CANAVARO: Kiiza acha kuchonga, tukutane uwanjani

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 21, 2015
  • 1 min read

Beki kisiki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, baada ya kusikia tambo za straika wa Simba, Mganda, Hamisi Kiiza, amemjibu kwa kumwambia aache kuchonga sana kwani watakutana uwanjani Jumamosi.

Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Kiiza ameanza kwa kusema atahakikisha anaifunga Yanga kwenye mchezo huo.

Cannavaro alisema anamheshimu Kiiza kutokana na uwezo wake, lakini atahakikisha anamzuia pindi watakapokutana katika mchezo wao.

“Nimesikia Kiiza anasema kwamba atatufunga, hilo asahau kabisa kwani tunajipanga kuhakikisha hakuna straika yeyote wa Simba atakayeupita ukuta wetu tukikutana Jumamosi.

“Tumejipanga kwelikweli kwani tunataka kuivunja rekodi ya kutopata ushindi kila tunapokutana na Simba kwa siku za karibuni, sasa ni zamu yetu,” alisema beki huyo wa kati ambaye kwa muda mrefu amekuwa akicheza pacha na Kelvin Yondani.

Katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara hadi sasa, Yanga imeruhusu bao moja tu kuzitikisa nyavu zake.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page