top of page

Bocco aing'alisha Azam 1, dhidi ya Mwadui 0 ya julio, Bahanunzi atakata manungu

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 21, 2015
  • 1 min read

BAO pekee la Nahodha John Raphael Bocco limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Azam FC inayofundishwa na Muingereza Stewart Hall, baada ya awali kushinda 2-1 dhidi ya Prisons Uwanja wa azam Comolex, Chamazi, Dar es Salaam na 2-0 dhidi ya Stand United Uwanja Kambarage, Shinyanga. Azam FC sasa inashuka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Simba SC, zikiwa na pointi sawa na Yanga SC, tisa kila moja, lakini zinazidiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. Katika mchezo wa leo, Azam FC ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Aggrey Morris kutolewa kwa kadi nyekundu, wakati mshambuliaji wa Mwadui FC, Rashid Mandawa alikosa penalti. Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar imeshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro mabao yake yakifungwa na Salum Mbonde na Said Bahanuzi la wageni likifungwa na Kiggi Makassy, wakati Coastal Union imelazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


 
 
 

Commentaires


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page