top of page

Yanga yaiadhibu TZprisons 3-0 taifa. Pichazzz>>>>

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 17, 2015
  • 1 min read

YANGA SC imeendelea kung’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 3-0 Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. Mabingwa hao watetezi, sasa wanafikisha pointi sita na mabao matano, baada ya awali kushinda pia nyumbani 2-0 dhidi ya Coastal Union. Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Mkongo, Mbuyu Twite dakika ya 27 baada ya kipa wa Prisons, Mohammed Yussuf kushindwa kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na Simon Msuva, kufuatia Deus Kaseke kuangushwa nje ya boksi.

Mrundi Amissi Tambwe aliifungia Yanga SC bao la pili dakika 45 akiumalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa Prison, Yussuf baada ya mpira wa adhabu wa kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima kufuatia Msuva tena kuangushwa. Mshambiliaji wa Prisons Jeremiah Juma alipoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza baada ya kupia juu la lango. Kipindi cha pili, kocha wa Prisons, Salum Mayanga alianza kwa kumpumzisha kipa Yussuf na kumuingiza Aron Kalambo Refa Alex Mahagi wa Mwanza alimtoa kwa kadi nyekundu James Josephat dakika ya 59 baada ya kumdondosha Msuva kwenye boksi na Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la tatu kwa penalti dakika ya 60. Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Haji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke/Salum Telela dk66 Simon Msuva, Haruna Niyonzima Geoffrey Mwashiuya dk79, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk84, Donald Ngoma na Deus Kaseke. Prisons: Mohammed Yussuf/ Aron Kalambo dk46, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, James Josephat, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sabianka, Juma Seif, Mohammed Mkopi/Cosmas Ader dk47, Boniface Hau Ally Manzi dk64 na Jeremiah Juma.


 
 
 

Comentários


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page