top of page

TFF yapeleka mbele uchaguzi Yanga, mpaka nchi impate raisi Oktoba

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 16, 2015
  • 1 min read

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema limepokea maombi ya klabu ya Yanga SC kutaka kufanya uchaguzi wake mkuu wa viongozi wa klabu hiyo kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya Utendaji. Hata hivyo, Taarifa ya TFF imesema wameiomba klabu hiyo kufanya mkutano wake wa Uchaguzi wa viongozi baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Rais, Wabunge na Madiwani) utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Hii ni kutokana na unyeti wa uchaguzi wa klabu ya Yanga yenye matawi nchini kote.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page