top of page

PLUIJM:Hatujakaa vizuri, lakin kazi mtaiona tuu

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 15, 2015
  • 1 min read

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ana imani na kikosi chake kuendelea kufanya vizuri ingawa kuna mambo kadhaa hajaridhika sana.

“Katika soka kila unapocheza, linaibuka jambo jipya. Mkirekebisha na kucheza mechi nyingine, linaibuka jambo ambalo linahitaji marekebisho tena.

“Huo ndiyo mpira, tulitengeneza nafasi nyingi dhidi ya Coastal. Tunachotakiwa ni kuzitumia zaidi,” alisema.

“Lakini kuna makosa kadhaa tulifanya, bado tutayafanyia kazi zaidi.”

Yanga imeanza kutetea kombe lake kwa kuichapa Coastal Union kwa mabao 2-0.

Mechi inayofuata Yanga itacheza na Prisons amnayo ilianza ligi hiyo kwa kipigo cha mabao 2-1 ktoka kwa Azam FC.


 
 
 

Comentários


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page