top of page

Yanga SC: Tumekamilisha taratibu zote za kuwasajiri Ngoma, Kamusoko na watakwepo dimbani kesho

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 12, 2015
  • 1 min read

YANGA SC imesema hakuna shaka wachezaji wake wote wa kigeni watacheza mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo mjini Dar es Salaam kwamba klabu imefuata taratibu zote kuhakikisha wachezaji wake wote wanacheza. “Nataka niwahakikishie wapenzi na wanachama wa Yanga SC kwamba wachezaji wetu wote wa kigeni wamekamilisha taratibu za usajili na watacheza Ligi Kuu kuanzia mwanzo,”amesema Dk. Tiboroha. Katibu huyo wa Yanga SC alikuwa anazungumzia madai kwamba wamekataa kuwalipia wachezaji wao ada ya dola za Kimarekani 2,000 (TSh. Milioni 4) kila mmoja hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewazuia. Wachezaji wa kigeni wa Yanga SC ni mabeki Mbuyu Twite kutoka DRC, Vincent Bossou kutoka Togo, viungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, Andrey Coutinho wa Brazil, Thabani Kamusoko, washambuliaji Donald Ngoma wa Zimbabwe na Amissi Tambwe wa Burundi. Yanga SC inatarajiwa kuanza kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Jumapili watakapoikaribisha Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page