Wanajeshi kuhudumia wakimbizi Ujerumani
- sembula
- Sep 12, 2015
- 1 min read

Wizara ya ulinzi nchini ujerumani inasema kuwa karibu wanajeshi 4000 wako tarayi kusaidia kukabiliana na karibu wakimbizi 40,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini humo.
Waziri wa ulinzi wa ujerumani alisema kuwa jeshi lilikuwa limejiandaa kutoa huduma za usafiri ikiwa itahitajika.
Hi leo Jumamosi maelfu ya watu wanaowaunga mkono wakimbizi wanatarajiwa kuandaa mikutano kwenye miji kadha ya nchi za ulaya.
Maandamano pia yatafanyika kupinga kuwasili kwa wakimbizi wengi.
コメント