GWAJIMA: "SLAA alikuwa Padri, akaacha na kuoa". Soma zaidi aliyoyasema Mch.Gwajima leo ku
- sembula
- Sep 8, 2015
- 2 min read
Siku chache baada ya aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaakutangaza kwamba ameamua kuachana na Siasa, baada ya siku kadhaa kutoonekana kwenye Mikutano pamoja na Viko vya CHADEMA pamoja na Vyama vya UKAWA, stori ambazo zinamtaja yeye bado hazijaacha kuibuka.
Kulikuwa na madai ambayo yaliripotiwa na Vyombo vya Habari pamoja na kuandikwa sana Magazetini na Mitandaoni pia ambapo Maaskofu walitajwa kuhusishwa na Rushwa… Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kaongea Dar es Salaam… kwenye alichokisema kuna hizi nukuu za alichokisema pamoja na pichaz pia.

'Lengo ni kufafanua maneno yaliyosemwa na rafiki yangu Dk.Wilbrod SLAA na kurushwa karibu kwenye TV zote'
Kati ya maneno yaliyonigusa ni kusema "GWAJIMA aliniambia Maaskofu walipewa Rushwa ili kumsapoti LOWASSA"-
Mara nyingi ananitaja mimi kuwa ni rafiki yake, siwezi kumkana kwa kuwa amekosea, ni rafiki aliyekosea'
Urafiki wangu na Dk. SLAA ulianza akiwa CHADEMA ktk Harakati za Ukombozi kuitoa nchi ktk matatizo'-
'Alipata matishio mengi ya kuuawa na kukamatwa, akaomba nimsaidie kumpa watu salama wa kumsaidia'-
'Nilimpa Walinzi wanne wa kumlinda, aliogopa kulindwa na Polisi au watu wengine angesalitiwa
Nilimpa Walinzi waaminifu waliokuwa wananilinda mimi, wamemlinda kwa zaidi ya miaka minne
'Nilimpa na mtu mwingine, mama mtu mzima wa miaka 50 akawa anampikia chakula nyumbani kwake
'Nitakayoongea kuhusu Dk. SLAA nayajua kuanzia jikoni, chumbani na ni ya uhakika kabisa'
Dk. SLAA alisema amehama CHADEMA kwa sababu ya ujio wa LOWASSA, sio kweli 'Ujio wa LOWASSA ulianza na Dk. SLAA mwenyewe, alikuja kuniomba nimsaidie wampate LOWASSA ili washinde Uchaguzi'-
'Mimi siko Kamati Kuu CHADEMA lakini niliomba niingie Kikao cha Kamati Kuu ili kuhakikisha LOWASSA amefika salama'-
Tulimaliza Kikao na SLAA saa sita usiku, baadaye nikaambiwa na Walinzi kuwa mke wa SLAA alimfungia nje'-
'Nilienda kwa SLAA akaniambia ameamua kujitoa kwenye Siasa kwa sababu Familia yake inavunjika'
Dk. SLAA alikuwa Padri hana uzoefu wa Ndoa, angalau sisi Wachungaji tunajua namna ya kuongoza ndoa'-Niliongea sana na mke wa SLAA amruhusu mume wake aendelee lakini aligoma'
'Dk. SLAA alisema kwenye Mkutano CHADEMA watu waliletwa na malori,mlioenda mtajibu kama SLAA ni mkweli au muongo'-
SLAA amesomeshwa na Kanisa Katoliki, leo anasingizia Maaskofu 30 wamepewa Rushwa ili waonekane hawafai''-
'Mimi ninasema Maaskofu wote hawakupewa Rushwa na hata mimi sikupewa'
Alisema kuna wakati nilizunguka na LOWASSA kwenye Ndege, nina Ndege yangu na ninaweza kupakia mtu yoyote'-
Anayemwongoza SLAA kutukana Maaskofu akome, kama watu wa Usalama mtaruhusu aendelee kutukana mimi nitakaa nae'-
SLAA alikuwa Padri, akaacha na kuoa, akiongea tena nitataja watoto wake ambao amewatelekeza na kuoa mke wa mtu'-
Comentários