Aliyeua simba Zimbabwe asema hakukosea
- sembula
- Sep 7, 2015
- 1 min read

Raia wa Marekani aliyewinda na kumuua Simba maarufu nchini Zimbabwe, Cecil, amesema hakutenda kosa lolote.
Daktari huyo wa meno Walter Palmer, aliyekabiliwa na shinikizo kubwa na maandamano yaliyopangwa na makundi ya kutunza mazingira amezungumzia swala hiyo kwa mara ya kwanza.
Daktari Palmer sasa anasema kuwa hakufahamu kuwa Cecil alikuwa maarufu kiasi hicho nchini Zimbabwe na kuwa laiti angelijuwa hangemuua.
''Laiti ningelijua kuwa huyo simba alikuwa ndiye Cecil singemuua'' Palmer aliiambia jarida la Minneapolis Star Tribune.
Image captionSimba huyo Cecil alikuwa ndiye nembo na kivutio cha watalii nchini Zimbabwe
''Hata baada ya kumuua hakuna kati yetu aliyefahamu kuwa alikuwa ndiye nembo na kivutio cha utalii nchini Zimbabwe, Hakuna kati yetu aliyefahamu kuwa alikuwa ni simba anayewasaidia watafiti wa mazingira kuelewa nyendo za wanyama pori kusini mwa Zimbabwe'' aliongezea daktari Palmer.
''Kama mnavyofahamu kumekuwa na tishio la usalama kwangu na kwa familia yangu lakini ninatarajia kurejea kazini wakati wowote sasa.
''Tukio hilo lililotokea mwezi Julai limeathiri pakubwa uwezo wangu kuendelea kutoa huduma kwa jamii na umma.''aliongezea daktari Palmer.
Zimbabwe imeitaka Marekani imrejeshe Palmer nchini humo iliajibu mashtaka yanayomkabili ya uwindaji haramu.
Image captionMaandamano makubwa yalisababisha akafunga zahanati yake Minnesota
Palmer ambaye ni mwenyeji wa Minnesota amekiri kwa mara ya kwanza kufyatua mshale uliomuua Cecil.
Hata hivyo anapinga madai kuwa walitumia bunduki kumuua zaidi ya saa 40 baada ya kumdunga mshale mara ya kwanza mbugani.
Palmer mwenye umri wa miaka 55 anadaiwa kulipa dola $50,000 ilikupata fursa ya kumwinda Cecil.
Comments