Wahamiaji zaidi kusafiri kwenda Austria
- sembula
- Sep 6, 2015
- 1 min read

Utawala nchini Austria unasema kuwa utatoa treni zaidi hii leo kusafarisha wahamiaji kutoka nchini Hungary ambapo wengi walikwama kwa siku kadha.
Takriban watu 10,000 wanaaminika kuingia nchini Austria siku ya Jumamosi wengine wakisafiri moja kwa moja kwenda nchini Ujerumani.
Umati wa watu ulikusanyika mjini Munich hiyo jana kuwashangilia wahamiaji hao walipowasili.
Ujerumani inasema kuwa kwa kulegeza kwa muda sheria za uhamiaji za muungano wa ulaya, imesaidia kuzuia janga la kibinadamu kati ya mpaka wa Hungary na Austria
Comments