top of page

Kocha Nigeria aukubali mziki wa Stars

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 6, 2015
  • 1 min read

Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh amesema hakutegemea kukutana na upinzani mkubwa kama alioupata katika kikosi cha Taifa Stars.

Stars inayofundishwa na Kocha mzalendo, Charles Boniface Mkwasa imeizuia Nigeria na kutoka nayo sare ya bila kufungana katika mechi ya kuwania kucheza Afcon iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Ilikuwa mechi ngumu sana kwetu kuliko nilivyotarajia, Tanzania walikuwa katika kiwango kizuri sana, jambo ambalo sikutegemea.

“Soka la Aftika linapiga hatua na kila sehemu mechi ni ngumu sasa. Lakini inatusaidia kujua kwamba hakuna utani na tunapaswa kujiandaa zaidi,” alisema Oliseh.

Stars ilionyesha kiwango cha juu katika mechi hiyo na nafasi nyingi za kumalizia kufunga zilipotea.

Stars ndiyo ilitawala mechi hiyo na kuipa Nigeria wakati mgumu sana.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page