top of page

Austria leo kupokea wahamiaji 10,000

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 5, 2015
  • 1 min read

Austria imesema inatarajia kupokea wahamiaji wapatao 10,000 wengi wao wakiwa wakimbizi kutoka Syria ambao wataingia katika nchi hiyo kutokea Hungary.

Usiku wa kuamkia leo wafanyakazi wa Shirika la misaada walipokea watu maelfu kwa maelfu baada ya nchi ya Hungary kutuma basi kuwachukua kutoka mpakani. Treni maalum zinawasafirisha kwenda Vienna.

Serikali ya Budapest imesema hakuna mabasi na treni zaidi ambapo makundi mengine ya watu wameanza kutembea kutoka mjini kuelekea kwenye mpaka wa Austria.

Ujerumani imesema nayo inatarajiwa wakimbizi wengi kuingia katika miji mbali mbali ya nchi hiyo


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page