top of page

Mwanajeshi apatikana na hatia ya dhuluma za ngono

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 4, 2015
  • 1 min read

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mwanajeshi mmoja wa kikosi chake cha kutunza amani, nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, kutoka Ufaransa amepatikana na hatia ya kumdhulumu kimapenzi msichana mmoja.

Kumekuwa na madai kadhaa kuwa wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa kutoka Ufaransa walihusika na kashfa ya kuhusika kimapenzi raia wa nchi hiyo kwa kuwahonga na chakula.

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja la kutetea haki za kibinadam, Zeid Ra'ad Al Hussein ambaye yuko ziarani nchini CAR, amethibitisha tukio hilo.

Amesema tukio hilo lilitokea mwaka uliopita na msichana hiyo alijifungua mtoto Aprili mwaka huu


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page