top of page

Enyema ajiondoa kutoka kikosi cha Nigeria

  • Writer: sembula
    sembula
  • Sep 3, 2015
  • 1 min read

Kipa wa Nigeria Vincent Enyema, amejiondoa kutoka kwa kikosi cha Nigeria, kitakachoshiriki katika mechi ya kufuzu kwa fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka wa 2017, dhidi ya Tanzania siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mamake.

Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh, amesema kwa sasa Enyema, amepata pigo kubwa na tumemruhusu kwenda nyumbani kwa misingi ya kibinadam.

Enyema alitarajiwa kusafiri Abuja siku ya Jumatatu, lakini alifutilia mbali safari hiyo.

Kipa wa timu ya Uingereza ya Wolves, Carl Ikeme, anatarajiwa kujaza pengo hilo katika mechi itakayokuwa ya kwanza katika timu hiyo ya Super Eagles.

Enyema, anayeichezea klabu ya Ufaransa ya Lille na mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Super Eagles, alikuwa kipa wa timu hiyo wakati ilipoicharaza Chad kwa magoli mawili kwa moja mjini Kaduna mwezi Juni mwaka huu.

Image captionKocha wa Nigeria Sunday Oliseh

Enyema ameichezea Nigeria mechi 101.

Misri ambayo haikushiriki katika fainali tatu zilizopita, iliishinda Tanzania 3-0 mjini Alexandria na sasa inaongoza kundi G, kutokana na wingi wa magoli.

Licha ya kuwa timu zinazoogopewa zaidi barani Afrika, Nigeria na Misri ambao ni mabingwa mara saba wa kombe hilo hawakufuzu kwa fainali iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea mapema mwaka huu.

Wakati huo huo, Shirikisho la mchezo wa Soka nchini Nigeria, NFF, limethibitisha kuwa Super Eagles itakwaruzana na Mena ya Jamuhuri Ya Niger, katika mechi ya kimataifa ya kirafiki tarehe 8 Septemba mjini Port Harcourt.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page