Chelsea yamtoa Moses Westham kwa mkopo
- sembula
- Sep 2, 2015
- 1 min read

Mshambuliaji Mnigeria aliyetemwa kwenye kikosi cha Nigeria na kocha mpya Sunday Oliseh kwa ajili ya kuivaa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ametupwa kwa mkopo West Ham United.
Septemba 5, Stars itacheza na Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya kuwania kucheza Afcon.
Huyo ni Victor Moses ambaye licha ya kusaini mkataba wa miaka minne na Chelsea, lakini kocha wake Jose Mourinho amekubali kumpeleka kwa mkopo West Ham.
Msimu uliopita, Moses alimaliza msimu akiwa kwa mkopo Stoke City. Safari hii alirejea na Chelsea ikampa mkataba mpya wa miaka minne lakini imeshangaza kwa kumuachia kwa mkopo tena.
Comments