IS walipua madhabahu Syria
- sembula
- Aug 31, 2015
- 1 min read

Wapiganaji wa dola ya kiislamu IS, wanadaiwa kulipua sehemu ya madhabahu ya kidini katika mji wa Syria wa Palmyra.
Kundi la kutetea haki za binadamu nchini Syria limesema kuwa wanamgambo hao wametumia mabomu kulipua hekalu ya kiroma ya Bel.
Image captionMadhabahu yakilipuliwa
Shirika hilo limesema kuwa uharibifu mkubwa umetokea baadha ya shambulio hilo.
Wiki iliyopita wanamgambo hao wameoneshwa aktika video wakilipua hekalu nyingine ya kale ya Baalshamin. Islamic State waliuteka mji wa Palmyra mwezi Mei na kuzua hofu ya kushambuliwa madhabahu hayo.

Comments