top of page

Winfried Bony aumia mguu, Atembelea magongo

  • Writer: sembula
    sembula
  • Aug 29, 2015
  • 1 min read

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Bony ataikosa mechi ya klabu yake, Manchester City dhidi ya Watford katika Ligi Kuu ya England baada ya kuumia mguu.

Mpachika mabao huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 28 kutoka Swansea City msimu uliopita ameposti picha katika akaunti yake ya Instagram leo akitembelea magongo na mguu wake umefungwa.

Na kocha wa Man City, Manuel Pellegrini amethibitisha Bony hatakuwepo uwanjani kesho, lakini atarejea uwanjani wiki itakayofuata baada ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika, akienda kuichezea Ivory Coast Septemba 5.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page