top of page

Watoto 163 waachiliwa na waasi CAR

  • Writer: sembula
    sembula
  • Aug 29, 2015
  • 1 min read

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF, limesema kuwa makundi yaliyojihami nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, yamewaachilia watoto mia moja sitini na watatu.

Watoto hao waliachiliwa mjini Batangafo, baada ya majadiliano kati ya shirika hilo na makundi hayo ya waasi mwezi Mei mwaka huu, kama sehemu ya mpango wa amani.

Tangu makubaliano hayo jumla ya watoto mia sita na hamsini wameachiliwa na makundi hayo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kati ya watoto elfu sita na kumi wanazuiliwa na makundi hayo ya waasi, wengi wao wakitumika kama wanajeshi, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza nchini humo mwaka wa 2013.


 
 
 

Kommentare


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page