Waandishi wa Al Jazeera kuhukumiwa Misri
- sembula
- Aug 29, 2015
- 1 min read

Mahakama nchini misri inatarajiwa kutoa hukumu yake hii leo kwenye kesi inayowakabili waandishi watatu wa kituo cha runinga cha Al Jazeera wanaotuhumiwa kwa kutangaza habari za uongo na kulisaida kundi la Muslim Brotherhood ambalo linatambuliwa kuwa kundi la kigaidi.
Waandishi hao wana matumaini kuondolewa mashtaka hayo baada ya hukumu za kwanza za kati ya miaka saba na kumi kupingwa na makundi ya kutetea haki za binadamu na serikali kadha.
Wawili kati ya waandishi hao ambao waliachiliwa kwa dhamana nchini Misri, Mohamed Fahmy and Baher Mohamed watarudi mahakamani kusikiza hukumu yao.
Mwandishi mwingine Peter Greste, yuko nje ya nchi baada ya kutimuliwa kutoka nchini humo mwezi Februari.
Comments