Askofu aliyekabiliwa na kesi aaga dunia
- sembula
- Aug 28, 2015
- 1 min read

Aliyekuwa Askofu wa kanisa la Katoliki kutoka Poland, ambaye alitarajiwa kufikishwa mahakamani kwa madai ya dhuluma za ngono amefariki.
Jozef Wesolowski alipelekwa hospitali mwezi uliopita, saa chache tu kabla ya kufishwa mahakamani.
Askofu huyo anatuhumiwa kuwapa watoto pesa na kuwadhulumu kingono wakati alikuwa balozi wa Vatican katika Jamuhuri ya Domincan.
Kamati maalum ya kanisa la Katoliki ilimpata na hatia na ikamsimamisha kazi mapema mwaka huu.
Wesolowski angelikuwa mtu wa kwanza wa ngazi ya juu katika kanisa hilo la Katoliki kufikisha mahakamani mjini The Vatican kwa madai ya kuwadhulumu watoto kingono.
Commenti