top of page

Yanga yaifuata Simba Z'bar

  • Writer: sembula
    sembula
  • Aug 27, 2015
  • 1 min read

Kikosi cha Yanga, kitakaa Zanzibar kwa siku 7 kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara

Zanzibar imekuwa ni maarufu kwa Simba kuweka kambi na tayari imeelezwa kwamba Simba inakwenda Zanzibar.

Yanga inaweka kambi Zanzibar baada ya ile kambi yake mkoani Mbeya.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema kambi yao itakuwa ni ya wiki moja.

"Wiki moja Zanzibar kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kwanza kwa ligi," alisema.

Yanga itacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara Septemba 13, itakuwa ni Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page