Polisi wanasa sehena ya Silaha Kenya
- sembula

- Aug 27, 2015
- 1 min read

Maafisa wa Ulinzi wa Kenya wamenasa shehena kubwa ya silaha, kufuatia operesheni ya kuwasaka wapiganaji wa Al Shabaab Kaskazini mwa Kenya.
Idara ya polisi imesema kuwa maafisa wake walinasa risasi, vilipuzi, bunduki na vifaa vinavyotumika kutengeneza mabomu ambazo zinaaminika kuwa ya wapiganaji wa Harakat walio na uhusiano na kundi la Al Shabaab nchini Somalia.
Wapiganaji kadhaa wa kundi hilo ambao walikuwa wakisafirisha silaha hizo, walikamatwa na wanazuiliwa na maafisa wa polisi.
Kundi hilo linasemekana kuwa na majukumu ya kuwasilisha na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wapya na hatya kujiunga na mapigano na mashambulio dhidi ya vituo vya umma.




Comments