top of page

Makundi UEFA haya hapa>>>

  • Writer: sembula
    sembula
  • Aug 27, 2015
  • 1 min read

Hatimaye msimu mpya wa wababe wa ligi za ulaya maarufu kama UEFA Champions League unakaribia kuanza, na jioni leo huko jijini Monaco yamepangwa makundi ya timu zitakazochuana kwenye michuano hiyo inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Kundi A, zimepangwa klabu ya Paris Saint Germain, Real Madrid, Shakhtar Donetsk na Malmo.

Kundi B, mabingwa wa mara 3 wa kombe hilo Manchester United wamerejea tena kushiriki kwenye michuano hiyo wakiwa wapo kwenye kundi linaundwa na PSV, CSKA Moscow na Wolfsburg ya Ujerumani.

Kundi C, litakuwa na timu za Benfica, Atletico Madrid, Galatasary na timu mpya kwenye michuano hiyo Astana ya Khazastan.

Kundi D, Linaundwa na waliocheza fainali msimu uliopita Juventus, Manchester City, Sevilla na Borussia Monchengladbach.

Mabingwa watetezi FC Barcelona watachuana na As Roma, Bayern Leverkusen na Bate katika kundi E.

Kundi F, litakuwa na timu za FC Bayern Munich, Arsenal, Olympiakos na Dinamo Zagreb.

Mabingwa wa Uingereza, Chelsea FC wanyewe wamepangwa katika kundi H ambalo lina timu za Porto, Dinamo Kyiv na Macabi Tel Aviv.

Kundi la mwisho linaundwa na Valencia, Zenit, Lyon na Gent, ambayo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page