top of page

Hii ni mipango ya FC Barcelona kuhusu Neymar kuhamia Man United

  • Writer: sembula
    sembula
  • Aug 27, 2015
  • 1 min read

Klabu ya Manchester United bado inasaka nyota kadhaa watakaojiunga na kikosi chao ili kuweza kuongeza nguvu na kucheza kwa kiwango cha juu. Man United ambayo kwa hivi karibuni ilimkosa Pedro Rodriguez baada ya kocha wa Chelsea Jose Mourinhokumpigia simu na kumshawishi ajiungea na Chelsea.

Sasa Man United wamerudi tena katika klabu ya FC Barcelona ila safari hii wanahitaji kumsajili nyota ambaye wengi wanaamini hawezi kuuzwa kipindi hiki. Inaripotiwa na vyombo vingi vya habari Uingereza kuwa Man United wanataka kumsajili Neymar na wametenga kiasi cha pound milioni 240 ili kumpata nyota huyo.

Stori zilizopo kwa sasa FC Barcelona wanajiandaa kumpatia Neymar mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya pound milioni 182, Mkataba ambao utamuweka NeymarNou Camp hadi mwaka 2023. Mkataba wa Neymar wa sasa utamalizika mwaka 2018.


 
 
 

Comments


RECENT POSTS:
SEARCH BY TAGS:

© 2023 by NOMAD ON THE ROAD. Proudly created with Wix.com

  • b-facebook
  • Twitter Round
  • Instagram Black Round
bottom of page